Vikwazo vya Iran kuondolewa
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amewasili mjini Vienna ambapo waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo vinatarajiwa kuondolewa hii leo.
Bwana Kerry anatarajia kukutana na waziri wa Mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ambaye pia yupo mjini Vienna hapo baadaye.
Shirika la uangalizi wa masuala ya Nyuklia la kimataifa IAEA linatarajia kutoa taarifa yake juu ya ukweli kuwa Iran imesimamisha uzalishaji wa mabomu ya nyuklia kwenye vinu vyake na makuabaliano ya serikali ya Tehran ya kuwekeza zaidi nyuklia yake itajikita zaidi kwenye matumizi ya amani.
Hatua hiyo itaifanya Iran iweze kufunguliwa kupata mabilioni ya fedha,mali na mauzo ya mafuta vyote ambavyo vilikuwa vimezuiwa na kuwekewa vikwazo kwa sababu ya muendelezo wake wa unurishaji wa vinu vya Nyuklia.
No comments:
Post a Comment